The Music Album That I Composed, Arranged, Sang and Performed at Age 15..

 

At the age of 15, I was able to transform my high school band, "TBC Band," which consisted of three members -- Joel Balisidya, James Sabuni, and myself -- by bringing in additional talent from Kinondoni Lutheran Church's Amkeni choir to record my first album ever, titled "Najiuliza."

 

The recording of this album was very challenging, as I was the youngest of all the members who participated and had to pay all costs from my school pocket money, though I borrowed some from my mom. The album did not come out as I wanted it to due to funds, the timing of other members who had their own personal and family issues, and my school. Thanks to God, one Sunday I went to the studio. I paid all the money the studio owed me and finalized the album by filling up all vocals and guitars, and I told the sound engineer to finalize and give me my master the same day without other members knowing.  

 

[Sound Engineer: Joseph Ananiah], [Vocals: Oscar Kulwa, Joshua Misonge, Godson Ruben, Joel Balisidya, Allen Kinsalla, and Dardan Mfalme], [Instruments: John Ndeki solo/lead guitar] Rhythm guitar/second solo - Dardan Mfalme. Bass guitar: Daniel Kisimbo Daniel Kulwa [Keys].

All songs were written, composed, and arranged by Dardan Mfalme.

 

You can listen to "Najiuliza album" here:    

 

 

 

[SWAHILI]

Nikiwa na umri wa miaka 15 tu, nilifanikiwa kuiboresha bendi yangu niliyoianzisha nikiwa shule ya sekondari kwa kuongeza vipaji toka kwenye kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kinondoni na kurekodi santuri yangu ya kwanza kabisa, inayoitwa Najiuliza.

 

Changamoto zilikua kubwa katika kurekodi kwani nilikua ni mdogo kati ya wadau wote waliohusika katika kurekodi santuri hii na pia ilibidi nilipie gharama zote kutoka kwenye akiba ya hela zangu za shule na nyengine nilizokopa kutoka kwa mama yangu. Santuri hii haikutoka kama nilivyotaka itoke kwa sababu ya uhaba wa fedha, muingiliano wa muda na wadau wengine waliokuwa na mambo yao binafsi na pia ratiba za masomo yangu. Namshukuru Mungu kwani kuna Jumapili moja nilipata hela nikaenda studio nikalipa hela zote walizokua wananidai na nikamalizia kujaza sehemu zote za sauti na gitaa zilizobaki na kumwambia fundi mitambo amalizie santuri yangu na kunikabidhi siku hiyo hiyo bila ya wadau wengine kujua.

 

Santuri hii imerekodiwa katika studio za Big Novemba - jengo la Umoja wa Vijana, Mnazi mmoja, Dar es Salaam. 

 

[Fundi Mitambo: - Joseph Ananiah], [Sauti: - Oscar Kulwa, Joshua Misonge, Godson Ruben, Joel Balisidya, Allen Kinsalla na Dardan Mfalme], [Vyombo: - Gitaa la solo - John Ndeki. Gitaa la kati - Dardan Mfalme. Gitaa la besi - Daniel Kisimbo. Kinanda - Daniel Kulwa].

Nyimbo zote zimetungwa, zimeandikwa na zimepangwa na Dardan Mfalme.